• HABARI MPYA

  Sunday, May 19, 2024

  TAIFA STARS YATOA SARE NA SUDAN 1-1 SAUDI ARABIA


  TIMU ya taifa ya Tanzania imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa King Fahd Sport City mjini Ta'if, Saudi Arabia.
  Bao la Taifa Stars inayoundwa na kikosi cha chipukizi wapya kabisa limefungwa na Oscar Adam Paul anayechezea Kakamega FC ya Kenya.
  Taifa Stars inakamilisha ziara yake ya mechi mbili za kujipima nguvu na Sudan kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mechi ya kwanza Mei 15 hapo hapo King Fahd Sport City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YATOA SARE NA SUDAN 1-1 SAUDI ARABIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top