• HABARI MPYA

  Wednesday, May 22, 2024

  AZİZ Kİ APIGA MBILI YANGA YAIBABUA DODOMA JIJI 4-0 JAMHURI


  MABINGWA, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Clement au Walid Francis Mzize kwa jina jipya baada ya kusilimu dakika ya 10 na viungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki mawili dakika ya 45’+4 kwa penaltı na dakika ya 51 na Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo, Yanga ambao tayari ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo na mara 30 jumla ambayo ni rekodi - wanafikisha pointi 74 katika mchezo wa 28, wakifuatiwa na Azam FC na Simba zenye pointi 63 kila moja.
  Kwa upande wao Dodoma Jiji baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 28 pia na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 12.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZİZ Kİ APIGA MBILI YANGA YAIBABUA DODOMA JIJI 4-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top