• HABARI MPYA

  Friday, May 24, 2024

  RAIS DK MWINYI AISHUKURU CAF KUIPA ZANZIBAR UENYEJI ASFC


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF) kwa kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya Ubingwa wa Soka kwa Shule za Afrika (ASFC) mwaka huu.
  Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk.Patrice Motsepe na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.
  Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendeleza na kudumisha uhusiano wake na CAF .
  Rais Dk.Mwinyi amemueleza Dk.Motsepe kuwa Zanzibar inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa kushirikiana na CAF.
  Rais wa CAF Dk.Motsepe leo atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS DK MWINYI AISHUKURU CAF KUIPA ZANZIBAR UENYEJI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top