• HABARI MPYA

  Saturday, May 04, 2024

  KYOMBO APIGA ZOTE MBILI SINGIDA YAIKANDA DODOMA 2-0


  WENYEJI, Singida Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao yote ya Singida Fountain Gate ambayo ipo chini ya kocha Ngawina Ramadhani Ngawina yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Habib Haji Kyombo la kwanza dakika ya nane na la pili kwa penalti dakika ya 77.
  Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 25 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Dodoma Jiji FC inabaki na pointi zake 28 za mechi 24 na kushukia nafasi ya 10 kutoka ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KYOMBO APIGA ZOTE MBILI SINGIDA YAIKANDA DODOMA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top