• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  MAN UNITED WAITWANGA MAN CITY 2-1 NA KUTWAA KOMBE LA FA


  TIMU ya Manchester United imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya waliokuwa wanashikilia taji hilo, Manchester City leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na mshambuliaji Muargentina, Alejandro Garnacho Ferreyra dakika ya 30 na kiungo Muingereza mwenye asili ya Ghana, Kobbie Boateng Mainoo dakika ya 39, wakati bao pekee na Manchester City limefungwa na mshambuliaji Mbelgiji Jérémy Baffour Doku dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Man United imelipa kisasi cha Fainali ya mwaka jana, ambayo Man City walishinda 2-1 Juni 3, mabao yote yake yakifungwa na kiungo Mjerumani, İlkay Gundogan dakika ya kwanza na 51, huku la Mashetani Wekundu  likifungwa na kiungo Mreno, Bruno Fernandes kwa penalti na dakika ya 33. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAITWANGA MAN CITY 2-1 NA KUTWAA KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top