• HABARI MPYA

    Monday, May 06, 2024

    AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MANUNGU


    TIMU ya Azam FC imeichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya yamefungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum dakika ya 20 na winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 65 na kwa ushindi huo Azam FC inafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga baada ya timu zote kucheza mechi 25.
    Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 17 baada ya kucheza mechi 25 pia na inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top