• HABARI MPYA

  Saturday, May 04, 2024

  JKT TANZANIA YAICHAPA GEITA GOLD 2-0 MBWENI


  WENYEJI, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya JKT Tanzania inayofundishwa na Kocha Malale Hamsini yamefungwa na Najim Magulu dakika ya 45’+3 na Daniel Lyanga dakika ya 56.
  Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 25 na kusogea nafasi ya nane, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 24 za mechi 25 pia nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA GEITA GOLD 2-0 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top