• HABARI MPYA

  Wednesday, May 15, 2024

  HAALAND APIGA ZOTE MBILI MAN CITY YAICHAPA SPURS 2-0 LONDON


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamejisogeza karibu na taji lingine la ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao yote ya Manchester City jana yalifungwa na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya 51 akimalizia pası ya kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne na dakika ya kwa penaltı  90'+1.
  Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mspaniola Pep Guardiola inafikisha pointi 88 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi pointi mbili Arsenal, wakati Tottenham Hotspur inabaki na pointi 63 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 37.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA ZOTE MBILI MAN CITY YAICHAPA SPURS 2-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top