• HABARI MPYA

  Thursday, May 16, 2024

  MAN UNITED YAICHAPA NEWCASTLE 3-2 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Mancheater United yamefungwa na washambuliaji, chipukizi wa umri wa miaka 19, Muingereza mwenye asılı ya Ghana, Kobbie Boateng Mainoo dakika ya 31, Muivory Coast Amad Diallo Traoré mwenye umri wa miaka 21 dakika ya 57 na Mdenmark Rasmus Winther Højlund dakika ya 84.
  Kwa upande wao Newcastle United mabao yao yamefungwa na washambuliaji Muingereza Anthony Michael Gordon (23) dakika ya 49 na bwana mdogo wa umri wa miaka 19, Lewis Kieran Hall dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi nane ilizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 37.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA NEWCASTLE 3-2 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top