• HABARI MPYA

  Friday, May 03, 2024

  AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF KWA KISHINDO


  TIMU ya Azam FC imekamilisha idadi ya timu nne za Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayotambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Namungo FC usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo, Muivory Coast Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 10, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 15, Feisal Salum Abdallah dakika ya 19 na Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 52, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na kiungo pia, Ayoub Semtawa dakika ya 45 na ushei.
  Azam FC sasa itamenyana na Coastal Unión katika Nusu Fainali ambayo juzi iliitoa Geita Gold kwa kuichapa bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Nusu Fainali nyingine ni baina ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Ihefu ambayo iliitoa Mashujaa FC kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 juzi pia Uwanja wa LITI mjini Singida.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF KWA KISHINDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top