• HABARI MPYA

  Tuesday, May 21, 2024

  AZAM FC YAIPIGA JKT TANZANIA 2-0 PALE PALE ISAMUHYO


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 30 na Feisal Salim Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 63 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa tayari, Yanga wenye pointi 71 za mechi 27 na mbele ya Simba yenye pointi 60 za mechi 27 pia.
  JKT Tanzania kwa upande wao baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 31 za mechi 28 na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA JKT TANZANIA 2-0 PALE PALE ISAMUHYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top