• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  FEI TOTO APIGA MBILI AZAM FC YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-1 CHAMAZI

  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 50, Kipre Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 65,na wazawa Feisal Salum Abdallah dakika ya 72 na 79 Iddi Suleiman 'Nado' dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 66, sawa na Simba SC na kuendelea kukamata nafasi ya pili kwa faida ya wastani wa mabao, huku Feisal akifungana kwa mabao kileleni na kiungo Mburkinabe wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki 18 kila mmoja kuelekea mechi za mwisho Jumanne.
  Kwa upande wake Kagera Sugar ambao lao pekee limefungwa na mshambuliaji mzawa pia Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 51 baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 31 katika mchezo wa 29 pia na kushukia nafasi ya 13.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Yanga imeichapa Tabora United 3-0, Simba imeichapa KMC 1-0, Singida imeichapa Geita Gold 2-1, Namungo imetoa sare ya 2-2 na Tanzania Prisons, Dodoma Jiji FC imewachapa wenyeji, Ihefu 2-0, Mashujaa imeichapa Mtibwa Sugar 3-2 na Coastal Union imetoa sare ya 0-0 na JKT Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEI TOTO APIGA MBILI AZAM FC YAICHAPA KAGERA SUGAR 5-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top