• HABARI MPYA

  Sunday, May 26, 2024

  MOROCCO AWATEMA SAMATTA NA JOB TAIFA STARS YA KUIVAA ZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA


  KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya wanaume, Hemed Suleiman ‘Morocco’ hajamjumuisha Nahodha, Mbwana Ally Sanatta katika kikosi cha wachezaji 34 cha Taifa Stars kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.
  Aidha, Morocco ameendelea kutomuita beki wa Yanga, Dickson Job baada ya kutofautiana naye wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast mapema mwaka huu kufuatia mchezaji huyo kukataa kucheza beki ya kulia akisistiza apangwe katikati.
  Tanzania imepangwa pamoja na Morocco, Zambia, Niger, Kongo na  Eritrea ambayo imejitoa katika Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
  Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.
  Taifa Stars inatarajiwa kushuka Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola kumenyana na Zambia katika mchezo wake wa pili wa kufuzu Kombe la Dunia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO AWATEMA SAMATTA NA JOB TAIFA STARS YA KUIVAA ZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top