• HABARI MPYA

  Friday, May 03, 2024

  RONWEN WILLIAMS AJITIA KITANZI MAMELODI HADI 2028


  KLABU ya Mamelodi Sundowns is imetangaza kumuongeza mkataba wa miaka minne kipa wake mzawa, Ronwen Williams ambao utamfanya adumu Chloorkop angalau mwaka 2028.
  Mkataba huo unatoa fursa kwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ aliyejiunga na Mamelodi Sundowns mwaka 2022 kuongeza mwaka mmoja zaidi.
  Ronwen Williams amekuwa na msimu mzuri akiiwezesha Mamelodi kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya DStv, African Football League (AFL) na kufuzu kwenye michuano ijayo ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
  Alifanya vizuri pia kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) akishinda Tuzo ya Kipa Bora wa michuano hiyo baada ya kuiwezesha Bafana Bafana kumaliza nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONWEN WILLIAMS AJITIA KITANZI MAMELODI HADI 2028 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top