• HABARI MPYA

  Monday, May 20, 2024

  MTIBWA SUGAR BADO KIDOGO TU KUIAGA RASMI LİGİ KUU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya bila mabao na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 21, ingawa inabaki nafasi ya mwisho katika ligi ya timu 16, wakati Namungo FC inafikisha pointi 32 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba baada ya wote kucheza mechi 28.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR BADO KIDOGO TU KUIAGA RASMI LİGİ KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top