• HABARI MPYA

  Sunday, May 05, 2024

  CHELSEA YA MOTO KABISA WEST HAM YAFA TANO MTUNGI


  WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Waingereza viungo Cole Palmer dakika ya 15, Conor Gallagher dakika ya 30, washambuliaji Chukwunonso Madueke dakika ya 36 na Msenegal Nicolas Jackson dakika ya 48 na 80.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 35 na kusogea nafasi ya saba, wakati West Ham United inabaki na pointi zake 49 za mechi 36 sasa nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YA MOTO KABISA WEST HAM YAFA TANO MTUNGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top