• HABARI MPYA

  Tuesday, May 14, 2024

  JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE 1-1 NA SINGIDA FG MBWENI

  WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jana Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo Mbweni, Dar es Salaam.  
  Mabao yote jana yalifungwa na kiungo Mghana, Nicholas Gyan anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, kwanza akiifungia timu yake dakika ya 66 na baada ye kujifunga dakika ya 87 kuipatia bao la kusawazisha JKT Tanzania.
  Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 31 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nane, wakati Singida Fountain Gate inafikisha pointi 30 nayo inapanda kwa nafasi moja hadi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 27.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE 1-1 NA SINGIDA FG MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top