• HABARI MPYA

  Monday, May 06, 2024

  LIVERPOOL YAICHAPA TOTTENHAM 4-2 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur usiku wa Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 16, beki Mscotland, 
  Andrew Robertson dakika ya 45, mshambuliaji Mholanzi, Cody Gakpo dakika ya 50 na kiungo Muingereza, Harvey Elliott dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 78 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 82 za mechi 35 na  vinara, Arsenal wenye pointi 83 za mechi 36, wakati Tottenham Hotspur inabaki na pointi zake 60 za mechi 35 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA TOTTENHAM 4-2 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top