• HABARI MPYA

  Saturday, May 11, 2024

  MAN CITY YAITANDIKA FULHAM 4-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND


  MABINGWA watetezu, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mabao ya Man City yamefungwa na beki Mcroatia, Josko Gvardiol (22) mawili dakika ya 13 na 71, huku mengine yakifungwa na kiungo Muingereza, Philip Walter Foden (23) dakika ya 71 na mshambuliaji Muargentina, Julian Alvarez (24) kwa penalti dakika ya 90'+6.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 85 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiizidi pointi mbili Arsenal baada ya wote kucheza mechi 36, wakati Fulham inabaki na pointi zake 44 za mechi 37 nafasi ya 14.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAITANDIKA FULHAM 4-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top