• HABARI MPYA

  Tuesday, May 21, 2024

  COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 PALE PALE KAITABA


  TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shadrack Mulungwe dakika ya 16 na Denis Modzaka dakika ya 69, wakati bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 73.
   Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 41, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 31 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 PALE PALE KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top