• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2012

  VINARA WA LIGI KUU KUJAZWA NOTI, MATAJI KESHOKUTWA DAR


  MABINGWA; Kikosi cha Simba msimu uliopita, kutoka kulia Okwi, Kaseja, Kapombe, Maftah, Kazimoto, Chollo, Uhuru, Yondan, Boban, Mafisango (marehemu) na Sunzu. Wengine ni Dk Kapinga wakati kocha Milovan amechuchumaa mbele. 

  Na Prince Akbar
  WADHAMINI wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo keshokutwa kwenye hoteli ya Double Tree Hilton mjini Dar es Salaam.
  Mfungaji bora, John Bocco atapokea kitita keshokutwa
  Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni.
  Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, na washindi wanaofuati, pia mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora nao watatuzwa.
  Wakati Simba iliibuka bingwa Ligi Kuu, Azam ilikuwa ya pili, Yanga ya tatu na John Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mfungaji bora, lakini mchezaji bora wa Ligi Kuu na kipa bora kitendawili kitateguliwa siku hiyo.
  Msimu uliopita kipa bora wa Ligi Kuu alikuwa Mghana, Yawe Berko wa Yanga, ambaye msimu huu kutokana na kuboronga kwa klabu yake, hapewi nafasi ya kutetea tuzo hiyo na zaidi haitakuwa ajabu Juma Kaseja wa Simba akiinua taji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VINARA WA LIGI KUU KUJAZWA NOTI, MATAJI KESHOKUTWA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top