TIMU ya Ihefu imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Mashujaa FC kufuatia sare ya 0-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
Kwa ushindi huo, sasa Ihefu itakutana na mshindi kati ya Yanga na Tabora United zinazomenyana usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment