• HABARI MPYA

  Monday, May 13, 2024

  YANGA MABINGWA TENA LIGI KUU TZ BARA MARA TATU MFULULIZO NA 30 JUMLA


  RASMI, Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 jumla baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la Charles Ilamfya dakika ya 32, kabla ya Yanga kutoka nyuma kwa mabao ya Mzambia Kennedy Musonda dakka ya 62, Nasry Kyombo aliyejifunga dakika ya 66 na Clement Mzize dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 71 katika mchezo wa 27 ambazo hakuna timu nyingine katika Ligi Kuu inayoweza kuzifikisha, hivyo kujihakikishia taji la ubingwa msimu huu, 2023-2024. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 20 za mechi 27 mkiani kabisa mwa Ligi Kuu. Sehemu pekee ya Mtibwa Sugar kujinusuru kutoshuka Daraja ni kwenye mchujo, Play-Offs kama itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Namungo nyumbani na Ihefu na Mashujaa ugenini na kumaliza nafasi ya 14 au ya 13. Na hiyo ni kama Geita Gold, Tabora United na Mashujaa hazitafanya vyema kwenye mechi zake tatu za mwisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA MABINGWA TENA LIGI KUU TZ BARA MARA TATU MFULULIZO NA 30 JUMLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top