• HABARI MPYA

  Friday, May 10, 2024

  COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA FG 2-0 MKWAKWANI


  WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagama (25) dakika ya 26 na kiungo Greyson Gerard Gwalala (30) dakika ya 46.
  Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 29 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA FG 2-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top