• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  AZAM FC FC YASAJILI KIUNGO MPYA MCOLOMBIA


  KLABU ya Azam FC imeendela kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kumtambulisha kiungo mpya, Ever Meza iliyemnunua kutoka klabu ya Leonnes ya kwao, Colombia.
  Meza, aliyezaliwa Julai 21, 2000; alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Alianza FC ya huko huko Colombia, amesaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka Azam Complex hadi mwaka 2028.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa tatu kusainishwa mkataba Azam FC hata kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa, baada ya beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien pia ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC FC YASAJILI KIUNGO MPYA MCOLOMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top