• HABARI MPYA

    Monday, May 06, 2024

    SIMBA SC YAICHAPA TABORA UNITED 2-0 CHAMAZI


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na kiungo wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 19 na mshambuliaji Edwin Balua dakika ya 77.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya tatu  nyuma ya Azam FC yenye pointi 57 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 65 baada ya wote kucheza mechi 25.
    Kwa upande wao Tabora United wanabaki na pointi zao 23 za mechi 25 sasa katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.
    Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA TABORA UNITED 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top