• HABARI MPYA

  Thursday, May 30, 2024

  AZAM FC YASAJILI MSHAMBULIAJI MWINGINE MCOLOMBIA


  KLABU ya Azam FC imemtambulisha mshambuliaji Jhonier Blanco, kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya Rionegro, kwao Colombia.
  Blanco aliyezaliwa Oktoba 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatuatia makubaliano baina ya klabu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia na Azam FC.
  Kisoka aliibukia akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas, baadaye akatolewa kwa mkopo klabu ya daraja la kwanza, Fortaleza. 
  Manbo yalimuendea vizuri Fortaleza akaibuka kuwa mfungaji bora akiisaidia kupanda daraja na alipomaliza uhamisho wake wa mkopo akarejea Aguilas Doradas na sasa anahamia Tanzania.
  Blanco anaungana na Wacolombia wenzake watatu, kiungo Ever Meza aliyesaini wiki iliyopita, beki Yeison Fuentes wote kutoka Leones FC ya kwao na mshambuliaji Franklin Navarro kutoka Cortulua ya nchini humo pia FC Colombia ambao walisajiliwa Januari mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI MSHAMBULIAJI MWINGINE MCOLOMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top