• HABARI MPYA

  Wednesday, May 22, 2024

  FAINALI KOMBE LA TFF AZAM NA YANGA KUPIGWA ZANZIBAR JUNI 2


  FAINALI ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup itafanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Juni 2 badala ya Uwanja wa Tanzanite uliopo Babati mkoani Manyara.
  Mchezo huo utazikutanisha timu za Azam FC na mabingwa watetezi, Yanga SC na sababu za kuuhamishia mchezo huo Zanzibar ni Babati kutokuwa na miundombinu rafiki kuhodhi mchezo mkubwa kama huo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI KOMBE LA TFF AZAM NA YANGA KUPIGWA ZANZIBAR JUNI 2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top