• HABARI MPYA

  Friday, May 17, 2024

  SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI FC 1-0 JAMHURI


  VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Muivory Coast Freddy Michael Koublan dakika ya saba akimalizia kazi nzuri ya winga Edwin Barua.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 60, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 27.
  Kwa upande wao Dodoma Jiji FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 27 nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16, ambazo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI FC 1-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top