• HABARI MPYA

  Friday, May 17, 2024

  KMC YAICHAPA SINGIDA FOUNTAIN GATE 1-0 CHAMAZI


  BAO pekee la mchezaji wa Kimataifa wa Somalia, Ibrahim Elias dakika ya 21 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 28 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa pointi mbili na Coastal Union ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 30 za mechi 28 nafasi ya 12.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho katika ligi hiyo ya timu 16 zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA SINGIDA FOUNTAIN GATE 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top