• HABARI MPYA

  Wednesday, May 08, 2024

  MUDATHIR ATOKEA BENCHI KUIPA YANGA USHINDI DHIDI YA KAGERA SUGAR


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 83 akimalizia pası ya kiungo mwenzake, Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso.
  Mudathir alifunga bao hilo dakika 10 tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua na kwa ushindi huo Yanga inafikisha pointi 68 katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 57 za mechi 25 na Simba SC pointi 53 za mechi 24.
  Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 26 pia nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR ATOKEA BENCHI KUIPA YANGA USHINDI DHIDI YA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top