• HABARI MPYA

  Tuesday, May 21, 2024

  SIMBA SC YAICHAPA GEITA GOLD 4-1 CHAMAZI


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza mawili dakika ya 45’+3 kwa penaltı na dakika ya 72 na mzawa, Ladack Chasambi dakika ya 86 na 90 +3 baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Geoffrey Julius dakika ya 11.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 63, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 28, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 25 za mechi 28 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA GEITA GOLD 4-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top