• HABARI MPYA

  Sunday, May 19, 2024

  AZİZ Kİ AIPELEKA YANGA FAINALI KOMBE LA TFF, IHEFU ‘YAFA KIUME’


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ‘CRDB Bank Federation Cup’ baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso dakika ya 101 akimalizia krosi ya mchezaji mwenzake wa zamani wa ASEC Mimosas, Peodoh Pacome Zouzoua kutoka upande wa kulia.
  Yanga sasa itakutana na Azam FC katika Fainali hayo yakiwa marudio ya Fainali ya msimu uliopita ambayo Wananchi walishinda 2-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Azam FC ilitangulia Fainali jana kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union mabao ya Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ mawili na Feisal Salum Abdallah moja Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZİZ Kİ AIPELEKA YANGA FAINALI KOMBE LA TFF, IHEFU ‘YAFA KIUME’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top