• HABARI MPYA

  Wednesday, May 01, 2024

  COASTAL UNION WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF


  TIMU ya Coastal Unión imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Mghana, Dennis Modzaka mwenye umri wa miaka 23 aliyefunga dakika ya 23 na sasa Wagosi wa Kaya au Wana Mangush watakutana na mshindi kati ya Azam FC na Namungo FC zitakazomenyana Mei 3 Jijini Dar es Salaam.
  Coastal Union inakuwa timu ya pili kutinga Nusu Fainali ya CRDB Bank Federation Cup baada ya Ihefu SC ambayo imeitoa Mashujaa FC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Ihefu itakutana na mshindi kati ya Yanga  na Tabora United zinazomenyana usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top