• HABARI MPYA

  Monday, May 27, 2024

  BIASHARA UNITED YAJISOGEZA KARIBU NA LİGİ KUU, MBEYA KWANZA KUJARIBU TENA MSIMU UJAO


  TIMU ya Biashara United imefuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuitoa Mbeya Kwanza kufuatia kuichapa 2-0 jana Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mabao ya Biashara United jana yalifungwa na Charles Lukindo na Abeid Athumani na kwa matokeo hayo Biashara United inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kuichapa Mbeya Kwanza 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Karume mjini Musoma.
  Biashara sasa itasubiri timu itakayoporomoka kutoka Ligi Kuu ikutane nayo katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao na atakayefungwa atacheza Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YAJISOGEZA KARIBU NA LİGİ KUU, MBEYA KWANZA KUJARIBU TENA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top