• HABARI MPYA

    Wednesday, May 08, 2024

    SERIKALI YAUSIMAMISHA UONGOZI NGUMI ZA KULIPWA


    WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ameusimamisha uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) kuanzia leo, Mei 8, 2024 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka.
    Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa imeeleza kwamba uamuzi huo umetolewa baada ya kikao baina ya Waziri Dk. Ndumbaro na viongozi wa Kamisheni hiyo na vyama vinavyounda Kamisheni hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma. 
    Katibu Mkuu Msigwa amesema kwamba kufuatia uamuzi huo, Waziri Dk. Damad Ndumbaro ameunda kamati ya mpito ya kuongoza TPBRC chini ya Mwenyekiti, Emmanuel Salehe, Makamu Mwenyekiti, Alex Galinoma, Katibu Mkuu Joseph Mpuya na Wajumbe Patrick Nyembela, Shaffi Dauda na Irene Mwasanga.
    Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri Dk. Damas Ndumbaro ameunda kamati ya kufanya uchunguzi kwa Kamisheni iliyosimamishwa kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoibuliwa na Wanachama wao ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa Katiba ya Kamisheni hiyo na mgongano wa maslahi.
    Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi Mmoja kuanzia Mei 8,2024 na itaongozwa na Mwenyekiti Christopher Kamugisha. Viongozi wengine ni Ingridy Kimario -Katibu, Mariam Aziz Fakii -Mjumbe na Sophia Alponary - Mjumbe
    Waziri Dk. Ndumbaro amewataka wadau wa michezo kote nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili azma ya Serikali ya kukuza na kuendeleza michezo itimie.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAUSIMAMISHA UONGOZI NGUMI ZA KULIPWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top