• HABARI MPYA

  Sunday, May 19, 2024

  USYK ASHINDA KWA POINTI ZA MAJAJI KUPISHANA, FURY ASEMA 'AMEBEBWA' KISA VITA


  BONDIA Oleksandr Usyk wa Ukraine usiku wa jana amesmshinda Muingereza Tyson Fury kwa pointi za majaji kupishana, 2-1 ukumbi wa Kingdom Arena Jijini Riyadh, Saudi Arabia na kuwa bingwa wa kwanza asiyepingika wa uzito wa juu wa mataji manne.
  Jaji mmoja tu alimpa ushindi Fury wa pointi 114-113, wakati wengine wawili walimpa Usyk ushindi wa pointi T115-112 na 114-113, hivyo kuwa bingwa mpya asiyepingika duniani uzito wa juu akihodhi mataji ya WBC, WBA, IBF na WBO. 
  Lilikuwa pambano la aina yake, Fury akianza kutawaka raundi za mwanzo, kabla ya Usyk kuzinduka baadaye na kufanikiwa hadi kumpeleka chini Gypsy King raundi ya tisa.
  Hata Hivyo, baada ya pambano hilo Fury alidai watu wanaegemea upande wa Usyk kwa sababu vita inayoendelea nchini kwao, Ukraine. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: USYK ASHINDA KWA POINTI ZA MAJAJI KUPISHANA, FURY ASEMA 'AMEBEBWA' KISA VITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top