• HABARI MPYA

  Monday, May 13, 2024

  TABORA UNITED YAICHAPA MASHUJAA 1-0 UWANJA WA MWINYI  BAO pekee la Eric Okutu dakika ya 70 jana liliipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14, wakizidiwa wastani wa mabao na Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi 27.
  Wapo mbele ya Geita Gold yenye pointi 24 nafasi ya 15 na Mtibwa Sugar pointi 20 nafasi ya mwisho, ya 16 baada ya wote kucheza mechi 26.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu zitashuka daraja na mbili nyingine, ya 13 na 14 zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kusalia Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAICHAPA MASHUJAA 1-0 UWANJA WA MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top