• HABARI MPYA

  Saturday, May 18, 2024

  AZAM YATINGA FAINALI KIBABE KOMBE LA TFF, YAITWANGA COASTAL 3-0


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inatambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. 
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman 'Sopu' (23) mawili dakika ya 42 kwa penalti na 79 na lingine Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' (26) dakika ya 68.
  Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili ya CRDB Bank Federation Cup baina ya mabingwa watetezi, Yanga na Ihefu SC zitakazomenyana kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YATINGA FAINALI KIBABE KOMBE LA TFF, YAITWANGA COASTAL 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top