• HABARI MPYA

  Friday, May 31, 2024

  KELVİN JOHN AJIUNGA NA TIMU YA ZAMANI YA MACHUPPA DENMARK


  MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Kelvin Pius John (20) amejiunga na klabu ya Aalborg BK ya Denmark kwa mkataba wa miaka minne kutoka KRC Genk ya Ubelgiji.
  Anakuwa Mtanzania wa pili kuchezea Aalborg BK baada ya Arhumani Iddi Machuppa aliyecheza kuanzia msimu wa 2007 hadi 2009 akıtumia jina la Mohamed Rajab.
  Akiwa Aalborg BK, Machuppa aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2008-2009 walipokuwa kundi moja, E na Manchester United ya England, Villarreal ya Hispania na Celtic ya Scotland.
  Man United na Villarreal zilisonga mbele huku Aalborg BK na Celtic zikitolewa.
  Kisoka, Kelvin aliibukia kituo cha Football House cha Mwanza mwaka 2015 kabla ya kuchukuliwa timu ya Vijana ya Taifa chini ya miaka 15, akapandishwa U17 na kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kabla ya kuchukuliwa na akademi ya Brooke House College ya Harborough, Leicestershire, England.
  Alicheza Brooke House College hadi mwaka 2021 alipochukuliwa na KRC Genk akianzia timu ya vijana U19 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2022 ambako amecheza jumla ya mechi 42 na kufunga mabao manne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KELVİN JOHN AJIUNGA NA TIMU YA ZAMANI YA MACHUPPA DENMARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top