• HABARI MPYA

  Thursday, May 16, 2024

  SIMBA SC WAWASILI MAKAO MAKUU YA NCHI KUIVAA DODOMA JIJI


  KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama Jijini Dodoma mapema leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, kesho Uwanja wa Jamhuri.
  Simba SC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 57 za mechi 26 nyuma ya Azam FC yenye pointi 60 za mechi 27, wakati Dodoma Jiji ina pointi 30 za mechi 26 nafasi ya 11.
  Na wote wapo nyuma ya mabingwa tayari, kwa mara ya tatu mfululizo, Yanga SC yenye pointi 71 za mechi 27.
  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAWASILI MAKAO MAKUU YA NCHI KUIVAA DODOMA JIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top