• HABARI MPYA

  Wednesday, May 22, 2024

  TABORA UNITED YAAMBULIA SARE KWA IHEFU 1-1 MWINYI


  WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Ihefu SC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia kabla ya beki Mkongo, Andy Bikoko Lobulka kuisawazishia Tabora United dakika ya 59.
  Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya 14, wakati Ihefu SC imefikisha pointi 33 na inabaki nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 28.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAAMBULIA SARE KWA IHEFU 1-1 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top