• HABARI MPYA

  Monday, May 06, 2024

  IHEFU SC YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 SINGIDA MABAO YA WAKENYA


  TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao yote ya Ihefu leo yamefungwa na Wakenya, mshambuliaji Elvis Baranga Rupia dakika ya 35 na kiungo Duke Ooga Abuya dakika ya 90’+3.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 11, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 27 na kushukia nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 25 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 SINGIDA MABAO YA WAKENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top