• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  NI AHLY MABINGWA TENA AFRIKA, WAICHAPA ESPERANCE 1-0 CAIRO


  TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Espérance Sportive de Tunis katika mchezo wa marudiano wa Fanali usiku huu Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
  Bao pekee la Al Ahly amejifunga kiungo Mtogo, Roger Ben Boris Aholou  dakika ya nne akijaribu kuokoa. Ikumbukwe mechi ya kwanza timu hizo kutoa sare ya bila mabao Mei 18 Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi Jijini Radès nchini Tunisia.
  Kwa kutwaa taji hilo la 12 la Ligi ya Mabingwa, Al Ahly watazawadiwa dola za Kimarekani Milioni 4, wakati Esperance watapata dola Milioni 2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AHLY MABINGWA TENA AFRIKA, WAICHAPA ESPERANCE 1-0 CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top