• HABARI MPYA

  Thursday, May 02, 2024

  BORUSSIA DORTMUND YAICHAPA PSG 1-0 SIGNAL IDUNA PARK


  BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Ujerumani, Niclas Fullkrug dakika ya 36 limewapa wenyeji, Borussia Dortmund ushindi wa 1-0 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Signal Iduna Park Jijini Dortmund nchini Ujerumani.
  Timu hizo zitarudiana Mei 7 Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Bayern Munich na Real Madrid.
  Ikumbukwe Bayern Munich na Real Madrid zilitoa sare ya 2-2 juzi Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani na zitarudiana Mei 8 Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid nchini Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORUSSIA DORTMUND YAICHAPA PSG 1-0 SIGNAL IDUNA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top