• HABARI MPYA

  Thursday, May 09, 2024

  SIMBA YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAICHAPA AZAM 3-0 FEI TOTO AKOSA PENALTI


  TIMU ya Simba SC imefufua matumani ya ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Dalili za mbaya kwa Azam FC zilijitokeza mapema tu dakika ya 35 baada ya kinara wa mabao wa timu hiyo, Feisal Salum Abdallah kukosa mkwaju wa penati uliogonga mwamba wa kulia kwa kipa wa Simba, Mmorocco Ayoub Lekred na kurejea uwanjani.
  Refa Ahmed Arajiga wa Manyara alitoa adhabu hiyo ya penalti baada ya beki Mcameroon wa Simba SC, Che Fondoh Malone Junior kumuangusha kwenye boksi winga wa kulia wa Azam FC, Mgambia Gibril Sillah.
  Kipindi cha pili Simba ikiongozwa na makocha wazawa, Juma Mgunda na Suleiman Matola ilikuja na mbinu mpya dhidi ya Azam FC inayoongozwa na makocha wageni, Msenegal Youssoupha Dabo na Mfaransa, Bruno Ferry na kufanikiwa kupata mabao matatu huku wakikosa mengine mawili ya wazi.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa viungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 63, Mkongo Fabrice Ngoma dakika ya 77 na beki mzawa, David Kameta 'Duchu' dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 56 katika mchezo wa 25, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi na wote wakiwa nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 68 za mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAICHAPA AZAM 3-0 FEI TOTO AKOSA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top