• HABARI MPYA

  Tuesday, May 14, 2024

  DURAN APIGA MBILI ASTON VILLA YATOA SARE 3-3 NA LIVERPOOL

  WENYEJI, Aston Villa usiku wa jana wametoa sare ya kufungana mabao 3-3 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Mabao ya Aston Villa yalifungwa na kiungo Mbelgiji, Youri Marion Tielemans dakika ya 12 na mshambuliaji Mcolombia, Jhon Jader Duran mawili dakika ya 85 na 88.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na kipa Muargentina, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya pili, winga Mholanzi Cody Mathes Gakpo dakika ya 23 na beki Muingerea mwenye asili ya Ghana, Jarell Amorin Quansah dakika ya 48.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 79, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Aston Villa inafikisha pointi 78 nayo inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 37.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DURAN APIGA MBILI ASTON VILLA YATOA SARE 3-3 NA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top