• HABARI MPYA

  Wednesday, May 29, 2024

  TAIFA STRAS YAENDA INDONESIA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA WENYEJI


  KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo kwenda Indonesia kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na wenyeji, Juni 2 kuanzia Saa 6:00 usiku Uwanja wa Madya Gelora Bung Karno Jijini Jakarta.
  Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji, Zambia Juni 11 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Zambia, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.
  Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STRAS YAENDA INDONESIA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA WENYEJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top