• HABARI MPYA

  Monday, May 20, 2024

  MASHUJAA YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE


  TIMU ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na David Ulomi dakika ya 14 na Mgandila Shaaban kwa penaltı dakika ya 20, wakati bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Omar Kindamba aliyejifunga dakika ya 63.
  Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 29, ingawa inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 33 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 28.
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHUJAA YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top