• HABARI MPYA

  Saturday, May 11, 2024

  NICOLAS JACKSON AIPIGIA LA USHINDI CHELSEA YAICHAPA NOTTINGHAM 3-2

   

  TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Ukraine, Mykhailo Mudryk (23) dakika ya nane, washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Raheem Shaquille Sterling (29) dakika ya 80 na Msenegal mzaliwa wa Gambia, Nicolas Jackson dakika ya 82.
  Kwa upande wao  Nottingham Forest mabao yao yamefungwa na beki Muivory Coast, mzaliwa wa Ufaransa, Willy-Arnaud Zobo Boly (33) dakika ya 16 na winga mwenye asili ya Ghana, Callum James Hudson-Odoi (23) dakika ya 74.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 29 za mechi 37 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NICOLAS JACKSON AIPIGIA LA USHINDI CHELSEA YAICHAPA NOTTINGHAM 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top